PICHA: Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo.
Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza.
Vera
aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa
kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema
ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe
hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano
ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.
Ndugu zake walipingana sana na wazo
lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati
walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho
Mmiliku wa
eneo la kuzikia liitwalo Eternal Garden Funeral home, Paulo Araujo,
aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote, kama mgeni maalumu.
Wakati akiwa ndani ya Jeneza mwanamke huyo alikua akifumbua macho na kufumba kama vile mtu aliyekufa na kufufuka.
Mwanamke huyo amesema alikuwa na ndoto ya
kulala kwenye Jeneza tangu miaka 14 iliyopita na hakuwa akifikiri
ingekuja kutokea akaitimiza, kwasasa amefurahi kutimiza
alichokitaka kabla hajafa.