Wednesday, 2 November 2016

Yanga wakubali kipigo cha pili msimu huu dhidi ya Mbeya City By Rama Mwelondo TZA on November 2, 2016 Share Tweet Share Share comments Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wao wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017. Yanga wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo chao cha kwanza kutoka Stand United cha goli 1-0 September 25 2016, leo November 2 2016 wamekubali kipigo cha pili kutoka kwa Mbeya City wakiwa katika dimba la Sokoine Mbeya. img-20161102-wa0049 Mbeya City wamefanikiwa kuifunga Yanga goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Mwasapili dakika ya 6 na Kenny dakika 36 goli ambalo lilichukua muda kidogo refa kufanya maamuzi kutokana na wachezaji wa Yanga kuligomea, Donald Ngoma ndio alifunga goli la kufutia machozi la Yanga dakika 4 za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko.

No comments:

Post a Comment